Wabeuzi na Wakosoaji
Lakini si kila mmoja yuko tayari kuchunguza ushahidi kwa makini. Bertrand Russell, anakubali kumwamini kwake Yesu hakuhusishwa na kweli za kihistoria.[4] Mwanahistoria Joseph Campbell, bila kunukuu ushahidi, kwa utulivu aliwaambia watazamaji wa televisheni ya PBS kwamba ufufuko wa Yesu ni tukio la kweli.[5] Wasomi wengine, kama John Dominic Crossan ya Semina ya Yesu, anakubaliana naye.[6] Hakuna mmoja wa hawa wabishi ameleta ushahidi wowote wa maoni yao.
Wakosoaji wakweli, tofauti na wabeuzi wabishi, wanavutiwa na ushahidi. Katika magazine ya Wakosoaji, tahariri iliyopewa jina “Mkosoaji ni Nani?” maelezo yafuatayo hutolewa: Ukosoaji ni… utumiaji wa mantiki kwa mawazo yote yoyote – hakuna tambiko la ng’ombe linaloruhusiwa. Kwa maneno mengine, wakosoaji hawaendi kwenye uchunguzi uliofunikwa kwa uwezekano kwamba jambo linaweza kuwa halisi au dai hilo linaweza kuwa kweli. Tunaposema sisi ni “wakosoaji” tunamaanisha lazima tuone ushahidi wa dhati kabla hatujaamini.[7]
Tofauti na Russell na Crossan, wakosoaji wengi wa kweli wamechunguza ushahidi wa ufufuko wa Yesu. Katika makala hii, tutasikia kutoka kwa baadhi yao na tuone jinsi gani wamechambua ushahidi kwa kile pengine ni muhimu katika historia ya maisha ya binadamu: Je Yesu kweli alifufuka toka katika wafu?
Unabii-Binafsi
Kabla ya kifo chake, Yesu aliwaambia wafuasi wake kwamba, angesalitiwa, angekamatwa na angesulubishwa na kwamba angerudi maishani siku tatu baadaye. Huo ni mpango wa ajabu! Kitu gani kilikuwa kinafuatia? Yesu hakuwa mbembelezaji tayari tayari kutenda kazi kwa ajili ya wengine kwa amri, badala yake aliahidi kwamba kifo chake na ufufuko wake utathibitisha kwa watu (ikiwa akili na mioyo yao ilikuwa wazi) kwamba Yeye alikuwa ni Masiha hasa.
Mwanafunzi wa Bibilia Wilbur Smith alielezea kuhusu Yesu:
“Wakati aliposema kwamba Yeye mwenyewe atafufuka tena toka katika wafu, siku ya tatu baada ya kusulubiwa, alisema kitu fulani ambacho ni mpumbavu peke yake angethubutu kusema, ikiwa alitegemea huduma zaidi za wafuasi wake, ingekuwa hana uhakika angefufuka. Hakuna muasisi wa dini yoyote ulimwenguni anayejulikana kwa watu amewahi kusema kitu kama hicho.”[8]
Katika maneno mengine, tangu Yesu alipowaambia wafuasi kwa uwazi kwamba angefufuka tena baada ya kifo chake, kushindwa kutimiza ahadi kungemfanya awe mwongo. Lakini tunaendelea mbele zaidi. Jinsi gani Yesu alikufa kabla hajafufuka tena?