Nje ya Uwezo wake
Fikiria kushinda bahati nasibu ya Powerball yenye tiketi moja tu miongoni mwa milioni zilizouzwa. Hebu sasa fikiria kushinda mamia ya bahati nasibu hizi katika mlolongo. Watu wangefikiria nini? Kabisa, “Ilipangwa!”
Na zaidi ya miaka mitatu dai kama hilo limefanywa na wakosoaji kuhusu utimizaji wa utabiri wa Agano wa Kale. Wamekubali kwamba ni kweli Yesu alitimiza utabiri wa kimasiha lakini wamemshtaki kwa kuishi maisha yake katika namna ambayo ya kutimiza utabiri kwa makusudi. Ubishi mzuri lakini si wa kukubalika kama inavyoweza kuonekana.
Angalia sifa za tabiri nne za kimasiha:
- Uzao wake ungetokea kwa Daudi (Yeremia 23:5).
- Kuzaliwa kwake kungetokea Bethlehem (Mika 5:2).
- Angehamia Misri (Hosea 11:1).
- Angeishi Nazareth (Isaya 11:1).[9]
Sasa, kitu gani Yesu angefanya kuhusu kutimiza tabiri hizi? Si yeye wala wazazi walikuwa na udhibiti wa uzao wake. Kuzaliwa kwake Bethlehem kulikuwa ni matokeo ya sensa iliyoamriwa na Kaizari Agusto. Kuhamia kwa wazazi wake Misri kulisababishwa na utesaji wa Mfalme Herod. Na mara Herod alipokufa, wazazi wa Yesu waliamua kuishi Nazareth.
Hata katika umri mdogo msanii Yesu aliangalia katika tabiri alizokuwa nazo kwa bahati alitimiza na aliamua kuzifuata na kuona kama angeweza kutimiza zilizobaki, (kama mtu fulani anavyoamua kulenga kimwezi kwenye mchezo wa karata wa Hearts), rundo la karata bado lingepangwa dhidi yake. Angalia baadhi ya sababu katika tabiri tulizokwisha angalia: Masiha angesalitiwa kwa vipande thelathini vya fedha; angeuawa kwa njia ya kusulubiswa; na watu wangepiga kura kwa ajili ya nguo zake. Hizi tabiri zote zikawa kweli kwa Yesu, lakini ni nguvu gani aliyokuwa juu ya utimizaji wa yoyote kati ya hizi?
Wasomi wa Biblia wanatuambia kwa karibu kumbukumbu 300 kwa tabiri maalum 61 za Masiha zilitimizwa na Yesu Kristo. Nafasi za wezekano kwa mtu mmoja kutimiza hizo tabiri nyingi ingekuwa ni zaidi ya uwezekano wa kihisabati. Isingeweza kutokea, hata muda kiasi gani ungetolewa. Kadirio moja la wanahisabati la hizo nafasi zisizowezekana ni “nafasi moja kati ya trilioni, trilioni, trilioni, trilioni, trilioni, trilioni, trilioni, trilioni, trillion, trilioni, trilioni, trilioni, trilioni.”[10]
Bertrand Russell, mtu mbishi asiyeamini Mungu yupo, aliulizwa katika mahojiano ya gazeti la Look, ushahidi gani ungetolewa kwake ili yeye aamini Mungu. Russell alijibu, “OK, ningesikia sauti toka angani na ikatabiri mfululizo wa vitu na vikatokea, kisha nahisi ningeweza kuamini kuna aina fulani ya kiumbe asiye wa kawaida”
Msomi wa Biblia Norman Geisler alijibu ubishi wa Russell. “Ningesema, ‘Mr Russell, kumekuwa na sauti toka mbinguni; imetabiri vitu vingi; na tumeviona bila ubishi vikitokea.’”[11] Geisler alikuwa akigusia ukweli kwamba kiumbe wa mbali nje ya dunia angeweza kutabiri matukio ya siku zijazo.