Yesu angeweza kuwa akidanganya?
Hata wakosoaji wakuu wa Yesu wamemwita mwongo. Kashifa hiyo kwa hakika haimfai Yesu mwenye maadili makuu na mafundisho ya hadhi ya juu. Lakini ikiwa Yesu si yule anayedai kuwa, lazima tuthibitishe uwezekano kwamba alikuwa akidanganya kila mtu kimataifa!
Mojawapo ya kazi za kisiasa zenye ushawishi mkuu za nyakati zote ziliandikwa na Niccolo Machiavelli in 1532. Katika msingi wake, Mwanamfalme Machiavelli anaaamini kwamba mamlaka, mafanikio, umaarufu na ufanisi, viko juu ya uaminifu, itikadi na uadilifu.
Ingewezekana Yesu Kristo angejenga kanisa lake katika uongo ili kupata mamlaka, umaarufu au mafanikio? Kwa kweli, wapinzani wa Yesu wa kiyahudi, walikuwa wakiendelea moja kwa moja kumfanya Yesu aonekane kama mwongo na tapeli!
Swali tunalotakiwa kushughulika nalo ni: Kitu gani kingeweza kumsukuma Yesu kuishi maisha yake yote kuwa mwongo? Alifundisha kwamba Mungu alipingana na kudanganya na unafiki, kwa hiyo asingekuwa akifanya hivyo kumfurahisha Baba yake. Kwa hakika hakudanganya kwa manufaa ya wafuasi wake, kwa sababu wote kasoro mmojawao walikuwa tayari kujitoa mhanga kuliko kukana ukuu wake. (Angalia “Je, Mitume waliamini Yesu ni Mungu? (Saa Andiko la Yesu) na kwa hiyo tunabakiwa na maelezo ya msingi ya namna mbili, na kila namna ni ngumu.