Aina gani ya Mungu?
Wengine wamebisha kwamba Yesu alikuwa tu akidai kuwa sehemu ya Mungu. Lakini nia ni kwamba sisi sote tu sehemu ya Mungu, na ndani yetu kuna mbegu ya utakatifu, hiyo si kwa urahisi kuwa ni maana inayowezekana kwa yale maneno na matendo ya Yesu. Mawazo hayo ni kudhania kimarejeo, na ni mageni/tofauti na mafundisho yake, tofauti na imani zake, na tofauti na uelewa wa wafuasi wake wa mafundisho yake.
Yesu alifundisha kwamba yeye ni Mungu katika namna ambazo wayahudi walimwelewa Mungu na namna ambayo maandiko ya waebrania yalivyomwelezea Mungu, sio kwa jinsi ambayo harakati za kizazi kipya kinavyomwelewa Mungu. Si Yesu wala wamsikilizao waliokatishwa kuona nyota, na wakati wanapomzunguzia, walikuwa hawazungumzii nguvu za anga. Kwa ufupi ni vibaya kuelezea upya kitu gani Yesu alimaanisha kuhusu Mungu.
Lewis anaeleza,
Sasa tuwe wawazi. Miongoni mwa waaminio utukufu wa Mungu wa ulimwengu, kama wahindi, yeyote aweza asema alikuwa sehemu ya Mungu, au aliyekuwa na Mungu, kwa sababu alikuwa myahudi, hakukumaanisha aina ya Mungu, kwa lugha yao, ilimaanisha Mungu kuwapo nje ya ulimwengu aliouumba na bila shaka alikuwa tofauti na kitu kingine chochote. Na unapoelewa hilo, utaona nini huyu mtu alichosema, rahisi kabisa, kitu cha kushangaza ambacho kimekuwa kikinenwa na midomo ya wanadamu.[19]
Bila shaka kuna hao ambao wanamkubali Yesu kama mwalimu mkuu, lakini hawataki kumwita Mungu. Kama mwamini Mungu, tumeona kwamba Thomas Jefferson alikuwa hana tatizo kukubali mafundisho ya Yesu ya maadili huku akikataa Uungu wake.[20] Lakini kama tulivyosema na tutavyochunguza zaidi, ikiwa Yesu hakuwa namna alivyodai kuwa, lazima tutafute sababu zingine ambazo hazikumfanya kuwa mwalimu mkuu wa maadili. Lewis alidai “Ninajaribu hapa kumzuia yeyote asije akasema kitu cha kipuuzi ambacho watu wengi wanasema kumhusu Yeye [Yesu]: “Mimi niko tayari kumkubali Yesu ni Mwalimu Mkuu wa Maadili, lakini sikubali dai lake la kuwa Mungu. ‘Hicho ni kitu kimojawapo tusichotakiwa kusema.”[21]
Katika kutafuta kwake ukweli, Lewis alijua kwamba hawezi kuwa na namna zote mbili za ukuu wa Yesu. Aidha Yesu alikuwa yule – Mungu aliyedai kuwa, katika mwili au madai yake hayakuwa kweli! Na kama hayakuwa kweli, Yesu asingeweza kuwa Mwalimu Mkuu wa Maadili. Angekuwa aidha anadanganya kimataifa? Au angekuwa mwendawazimu akidai namna mbalimbali za Uungu.