Mwalimu wa Maadili Mkuu?
Hata hao toka katika dini zingine wanakiri kwamba Yesu alikuwa Mwalimu wa Maadili Mkuu. Kiongozi wa wahindi, Mahatma Gandhi, aliongelea mno maisha ya Yesu na maneno yake makuu ya busara.[1] Vile vile msomi wa Kiyahudi Joseph Klausner aliandika, “Inakubalika pote kwamba Kristo alifundisha maadili safi na makuu matukufu… ambayo yanapita mafundisho na maneno ya watu wa busara wa kale, yakiwafunika.”[2]
Mafundisho ya Yesu mlimani, yameitwa ni mafundisho bora ya binadamu, yaliyowahi kutamkwa na binadamu. Kwa kweli, mengi ya tujuayo leo kama “haki sawa” kwa kweli ni matokeo ya mafundisho ya Yesu. Mwanahistoria Will Durant, si-Mkristu, alisema kwamba Yesu aliishi na alipambana vilivyo bila kukoma kwa ajili ya ‘haki sawa’ katika nyakati za sasa angepelekwa Siberia. YEye ambaye ni mkuu miongoni, mwache awe mtumishi wenu” hii ni kinyume na maono ya kisiasa ya ufahamu wote.[3]
Wengi kama Ghandi, wamejaribu kutofautisha mafundisho ya Yesu ya maadili kutoka katika madai yake kuhusu yeye mwenyewe, wakiamini alikuwa ni mtu tu mkuu ambaye alifundisha maadili lukuki – mengi. Hii ilikuwa ni njia ya mmoja wa Baba Waasisi, Rais Thomas Jefferson, ambaye alikariri na kunakili Agano Jipya, akiondoa sehemu zilizomzungumzia Uungu wa Yesu, akiacha vifungu vilivyojali mafundisho ya kiimadili ya Yesu.[4] Jefferson aliendelea na kukopi kwake na kunakili Agano jipya akimheshimu Yesu kama labda ni mwalimu mkuu kuliko wote wa maadili wa nyakati zote.
Kwa hakika, maneno ya kukumbuka ya Jefferson katika Tangazo la Uhuru yalijengwa ndani ya misingi ya mafundisho ya Yesu kwamba kila mtu ni wa umuhimu mkubwa na sawa kwa Mungu, bila kujali jinsi, taifa, rangi wala nafasi yake katika jamii. Andiko maarufu laweka wazi, “Twashikilia kweli hizi kuwa ushahidi kwamba watu wote wameumbwa sawa, kwamba wamebarikiwa na Muumbaji kwa haki fulani sawa zisizohamishika na zisizotwalika/twaliwa na mtu mwingine…”
Lakini kitu kimoja Jefferson hakukijibu: Ikiwa Yesu si kweli alidai kuwa Mungu, asingekuwa mwalimu mzuri wa maadili. Lakini ni kweli Yesu alidai Uungu? Kabla hatujaangalia kitu gani Yesu alidai, twahitaji kuchunguza uwezekano kwamba alikuwa tu kiongozi mkuu wa dini?