Yesu angeweza kuwa anajidanganya mwenyewe?
Albert Schweitzer, ambaye alitunukiwa Nishani ya Nobeli mwaka 1952 kwa juhudi zake za kibinadamu, alikuwa na maoni yake binafsi kuhusu Yesu. Schweitzer alidai kwamba uendawazimu uliambatana na madai ya Yesu, kudai kuwa Mungu! Kwa maneno mengine, Yesu hakuwa sahihi kuhusu madai yake lakini hakudanganya kimataifa. Kulingana na nadharia hii ya kubuni, anadai Yesu alijidanganya hadi kufikia hatua ya kuamini alikuwa Masiha!
Lewis anafikiria wazo hili kwa makini sana. Anachambua kwamba ikiwa madai ya Yesu hayakuwa kweli, basi lazima alikuwa mwendawazimu. Lewis anatoa sababu kwamba kama mtu aliyedai kuwa Mungu asingekuwa mwalimu mkuu wa maadili, angekuwa aidha mwendawazimu sawa na mtu anayesema yeye ni yai, au vinginevyo angekuwa ni shetani wa Jehanam.[24]
Wengi wamesoma maisha na maneno ya Yesu na wamemkiri kwamba ni mtu tu mwenye busara sana. Ingawaje maisha yake mwenyewe yalishutumiwa na upotofu na ukosoaji binafsi, mwanafalsafa maarufu wa kiFaransa Jean Jacques Rousseau (1712 – 78) amekiri tabia kuu takatifu ya Yesu na yenye akili timamu akisema “Wakati Plato alipoelezea kuwa Yesu ni mwenye haki, alielezea tabia halisi ya Yesu. Ikiwa maisha na kifo cha Socrates ni yale ya huyo mwanafalsafa, basi maisha na kifo cha Yesu ni yale ya Mungu.”[25]
Bono anahitimisha kwamba ‘mwendawazimu” ndio kitu cha mwisho ambacho mtu angemdhania Yesu kuwa.
“Hivyo kitu unachobakia nacho ni aidha kusema Kristo alikuwa ndivyo alivyosema, alikuwa ndiye, au mwendawazimu. Ninamaanisha, tunasema mwendawazimu katika dhana ya Charles Manson…. Sitanii hapa. Wazo kwamba maendeleo yote ya ustaarabu kwa zaidi ya nusu ya dunia yangeweza kubadilika ama kubadilishwa na mwendawazimu! Kwangu mimi huo ni uongo uliozidishwa kipimo.”[26]
Eti kwamba Yesu alikuwa mwongo au mwendawazimu, kwamba alikuwa ni Mtoto wa Mungu? Jefferson angekuwa sahihi kumwita” Yesu mwalimu wa maadili pekee” huku akina uungu wa Yesu? Kitu cha kufurahisha, watu waliomsikia Yesu wote, wafuasi na maadui zake hawakuwahi kumfikiria Yesu kuwa ni mwalimu tu maadili. Yesu amepata mambo matatu kwa watu waliokutana nao: chuki, vitisho au kuabudiwa.
Madai ya Yesu yametulazimisha kuchagua. Kama ambavyo Lewis alivyonena, hatuwezi kumweka Yesu katika kundi la kuwa tu ni kiongozi mkuu wa dini or mwalimu wa maadili. Ukosoaji huu wa kizamani unatupa changamoto kusafisha akili zetu kuhusu Yesu,
“Lazima ufanye uamuzi wako sasa. Aidha huyu mtu alikuwa, au ni mwana wa Mungu: au vinginevyo ni mwendawazimu au ni kitu kingine. Unaweza kumnyamazisha Yesu kwa kumfanya mpumbavu, unaweza kumtemea mate, kumuua kama pepo au unaweza kuanguka miguuni pake Yesu na kumwita Bwana na Mungu. Lakini tusilete upuuzi wowote wa kumdhalilisha Yesu kuwa ni mwalimu tu mkuu mwanadamu. Hajaacha hivyo wazi kwetu. Hakukusudia hivyo.”[27]
Katika ukristu pekee, Lewis amechunguza wazo linalotafakari utambulisho wa Yesu, akihitimisha kwamba Yesu kwa hakika yuko vile vile alivyodai kuwa. Uchunguzi wake makini wa maisha na maneno ya Yesu ulipelekea huyu mtu mwerevu akane imani yake ya zamani ya kutoamini na akaongoka kuwa mKristu wa kweli dhati anayeamini.
Swali kuu katika historia ya mwanadamu ni, “ni nani ni Yesu Kristo wa kweli?” Bono, Lewis na wengine wengi wasiohesabika wamehitimisha kwamba Mungu alitembelea sayari katika umbo la mwanadamu. Lakini kama hivyo ni kweli, basi tungemtarajia kuwa hai leo. Na hivyo ndivyo ilivyo kwa hakika na jinsi wafuasi wake wanavyoaamini.
Ni kweli Yesu alifufuka toka katika Wafu?
Mashahidi wa macho kwa Yesu Kristo kwa kweli walizungumza na walitenda kama walivyoamini, alifufuka toka katika wafu baada ya kusulubiwa kwake. Ikiwa walikosea basi uKristu umeanzishwa kwa uongo? Lakini kama walikuwa sahihi, muujiza huo ungethibitisha yote Yesu aliyosema kuhusu Mungu, kuhusu yeye na kutuhusu sisi.
Lakini ni lazima tuamini ufufuko wa Yesu Kristo kwa imani pekee, au kuna ushahidi wowote wa kihistoria? Wakosoaji kadhaa walianza uchunguzi kwenye kumbukumbu za kihistoria kujaribu kuona kama kweli maelezo ya ufufuko yalikuwa uongo. Kitu gani waligundua?
Kuangalia ushuhuda wa madai makuu yaliyowahi kufanyika ya ufufuko wa Yesu Kristo!
Bonyeza hapa kwa ajili ya kudai zaidi fantastic milele alifanya – ya ufufuo wa Yesu Kristo!
« Previous | Next »