Sifa Za Yesu
Umeshawahi kukutana na mtu ambaye ni nguvu ya kusikilizwa mahali pote aendapo? Baadhi ya sifa za mafumbo, zisizoelezeka kirahisi zimemtenga mbali na watu wengine wote. Kwa hakika, hivyo ndivyo ilivyokuwa miaka elfu mbili iliyopita kwa Yesu Kristo, lakini hiyo haikuwa tu tabia ya Yesu pekee iliyowavuta hao waliomsikia. Kwa hao walioshuhudia maneno na maisha yake wanatuambia jambo fulani kuhusu Yesu wa Nazareti kuwa alikuwa tofauti na watu wengine wote.
Sifa pekee za Yesu zilikuwa ni yeye mwenyewe. Hakuandika kitabu, hakuamrisha jeshi, hakushikilia ofisi ya kisiasa, wala hakumiliki mali. Hasa, alisafiri karibu maili mia moja za kijiji chake, akiwavuta makundi ya watu walioshangazwa kwenye maneno makali na matendo yake ya kushangaza.
Na pia ukuu wa Yesu ulikuwa wazi kwa hao waliomuona na kumsikiliza. Na wakati watu wengine maarufu hatimaye husahaulika kwenye vitabu vya historia, Yesu bado ni kitovu cha maelfu ya vitabu na majadiliano yasiyo na kifani kwenye vyombo vya habari. Na mengi ya majadiliano hayo yanazungukia kuhusu madai ambayo Yesu aliyafanya – madai ya msingi ambayo yaliwashangaza wote, wafuasi wake na maadui zake.
Hasa ni madai ya kipekee ya Yesu yaliyomsababishia aonekane kama tishio kwa Mamlaka za Kirumi na Tawala za Kiyahudi. Japokuwa alikuwa mgeni asiye na sifa wala nguvu za kisiasa, lakini ndani ya miaka mitatu, Yesu amebadilisha dunia kwa karne 20 zingine zijazo. Viongozi wengine wa kimaadili na kidini wameacha mfano – lakini si kama huo wa mtoto huyo wa Seremala wa kawaida kutoka Nazareti.
Ni kitu gani kuhusu Yesu Kristo ambacho kimeleta mabadiliko? Alikuwa ni mtu mkuu tu, au kuna kitu cha zaidi?
Maswali haya yaelekea kwenye kiini kwamba Yesu alikuwa ni nani hasa. Wengine wanaamini alikuwa tu ni mwalimu wa maadili makuu; wengine wanaamini alikuwa ni kiongozi tu wa dini kubwa duniani. Lakini wengine wanaamini zaidi ya hayo. Wakristu wanaamini kuwa Mungu kwa hakika alitujia duniani katika umbo la ubinadamu. Na wanaamini kwamba ushahidi unathibitisha hilo.
Baada ya kuchunguza kwa makini maisha na maneno ya Yesu, Profesa wa zamani wa Oxford na Mdadisi C.S. Lewis, aliishia kwenye hitimisho la kushangaza kumhusu yeye kiasi kwamba alibadilisha mwenendo wa maisha yake.
« Previous | Next »