Kosozi za mwanzo
Kinyume na madai ya Brown, haikuwa Constantine aliyefanya imani za Kinostiki(Imani ya Uficho) kuwa pinzani; ilikuwa ni mitume wenyewe. Mazoea kidogo yaa falsalfa yalikuwa tayari yanakua katika karne ya kwanza, miongo kadhaa ya kifo cha Yesu.. Mitume katika mafundisho na maandiko yako, walienda mbali kulaumu imani hizi kwamba zimepingana na ukweli wa Yesu, kwake yeye ambaye walikuwa mashahidi wa macho.
Angalia, kwa mfano, kile mtume Yohana aliandika karibu mwisho wa karne ya kwanza:
“Nani ni mwongo mkubwa”? Anayesema kwamba Yesu si Kristo. Watu hao ni wapinga Kristo, kwa sababu wamemkana Baba na Mwana.” (1 Yohana 2:22)
Likifuata mafundisho ya mitume, viongozi wa kanisa la mwanzo kwa pamoja wakalaumu mafundisho ya Kinostiki ya siri ya wachache kuwa ni kidhehebu-tenge. Padri wa Kanisa Irenaeus, akiandika miaka 140 kabla ya Baraza la Nicaea, alihakikisha kwamba Wanostiki walilaumiwa na kanisa kama wapinzani. Pia alizikataa “injili” zao. Vile vile, akirejelea kwenye Injili nne za Agano Jipya, alisema, “Haiwezekani kwamba Injili zinaweza kuwa zaidi au chache katika idadi kuliko zilivyo.” [9]
Mwanateolojia Origen aliandika hili katika karne ya tatu, zaidi ya miaka mia moja kabla ya Nicaea:
Najua injili fulani ambayo inaitwa “Injili kulingana na Thomaso” na “Injili kulingana na Mathayo”, na nyingi nyinginezo tulizosoma – tusifikiriwe kwa njia yoyote wajinga kwa sababu ya hao wanaofikiri wanamiliki elimu fulani ikiwa wamejulishwa haya. Hata hivyo, miongoni mwa yote haya tuliyothibitisha pekee ambayo kanisa limetambua, ambalo ni kwamba Injili nne tu zinapaswa kukubaliwa.[10]
Hapo tunayo katika maneno ya kiongozi wa kanisa anayeheshimiwa sana. Wanostika (Wenye Elimu-Ficho) walitambuliwa kama dhehebu lisilo la kikristo barabara kabla ya Baraza la Nicaea. Lakini kuna ushahidi zaidi unauliza madai yaliyofanywa katika Maandiko ya Da Vinci.
Nani ni mbaguzi wa kijinsia?
Brown anapendekeza kwamba mojawapo ya vichocheo kwa ajili ya kupiga marukufu maandishi ya kinostiki (ya wachache) na Constantine kunakosemekana ilikuwa ni tamaa ya kukandamiza wanawake katika kanisa. Kinyume chake kikejeli, ni Injili baguzi ya Thomas ambayo inadhalilisha wanawake . Inahitimisha (kulingana na hali ikimnukuu Peter) pamoja na kauli hii ya kushangaza: “Mwacheni Maria aende mbali nasi, kwa sababu wanawake hawana thamani na maisha” (114).[11] Kisha Yesu kama inavyodaiwa akamwambia Petro atamfanya Maria awe mwanamme ili aweze kuingia katika ufalme wa mbinguni. Soma: wanawake ni duni. Kwa fikira kama hizo zinazooneshwa, ni vigumu kuelewa maandiko ya Kinostiki ya wabaguzi wachache kuwa ni mapambano kwa ajili ya kuwakomboa wanawake.
Kwa kinyume kabisa, Yesu wa injili za Kibiblia siku zote amekuwa akiwatendea wanawake kwa utu na heshima. Aya endelevu za kimageuzi kama hii mojawapo ndani ya Agano jipya zimekuwa ni msingi kwa majaribio katika kuinua hadhi ya wanawake:
“Hakuna tena myahudi au mtaifa, mtumwa au mtu huru, mwanamme au mwanamke. Kwenu ninyi wakristu- ninyi ni wamoja katika Kristo Yesu” (Wagalatia 3:28, NLT).