Wacha tukubali kwa muda kwamba mapendekezo ya Teabing yanaweza kuwa kweli. Kwanini kwa hali hiyo Halmashauri ya Nicaea iliamua kumtukuza Yesu kwa utakatifu?
“Ilikuwa hivyo kwa ajili ya mamlaka, ” Teabing anaendelea. “Kristo kama Masiya alikuwa muhimu kwa utendajikazi wa Kanisa na nchi. Wanafunzi wengi wanadai kwamba Kanisa la kwanza kwa kweli lilimwiba Yesu kutoka kwa wafuasi wake halisi, likiteka taarifa zake za kibinadamu, likazificha ndani ya la vazi la dini, na likazitumia kupanua mamlaka yake.”[4]
Kwa namna nyingi, Maandishi ya Da Vinci ni nadharia ya mwisho ya kushiriki hila Ikiwa madai ya Brown ni sahihi, basi tumekuwa tukidanganywa na kanisa, na historia na Biblia. Labda hata na hao tuwaaminio zaidi: wazazi wetu au walimu wetu. Na yote yalikuwa ni kwa ajili ya kutwaa mamlaka.
Ingawaje Siri za Da Vinci ni za kutunga, hazijengi sana dhana yake kwenye matukio ya kweli (Halmashauri ya Nicaea), watu halisi (Constantine na Arius), na nyaraka halisi (Injili za Kiroho). Ikiwa tunapaswa kujua kwa kina kuhusu hila hizi, kazi yetu ni lazima kushughulikia madai ya Brown na kutengananisha ukweli mbali na kutunga.
Constantine na Ukristo
Katika karne kabla ya utawala wa Constantini kwa Kimaya ya Kirumi, wakristu walikuwa wakiteswa sana. Lakini pia, wakati akijiimarisha katika vita, Constantine aliripoti kuwa ameona nuru angavu ya msalaba angani iliyochorwa na maneno “Shinda kwa hii.” Aliingia katika mapambano chini ya ishara ya msalaba na alichukua utawala himaya.
Kubadili kwa wazi kwa Constantine kuingia Ukristu kulikuwa ndio eneo kutofautiana katika historia ya kanisa. Roma ikawa ni himaya ya Kikristo. Kwa mara ya kwanza kwa karibu miaka 30, ikawa salama kiasi, na safi kuwa mkristo.
Wakristu hawakuteswa tena kwa imani yao. Constantini kisha akatafuta kuunganisha Himaya za Mashariki na Magharibi ambazo ziligawanywa vibaya kwa itikadi, imani, taratibu, akaleta habari ya utambulisho wa Yesu Kristo.
Hizi ni baadhi baadhi ya vyombo vya ukweli katika Siri za Da Vinci,na vyombo vya ukweli ni utangulizi kwa wazo lolote la hila za mafanikio. Lakini hila za kitabu zinamgeuza Constantine kuwa mshiriki-hila. Kwa hiyo tushughulikie suala muhimu la msingi lililoletwa na nadharia ya Brown; je Constantine ndiye alivumbua imani wa kikristo ya utakatifu wa Yesu?