Hila za Yesu
Siri za Da Vinci zinaanza na mauaji ya mtunza nyumba ya makumbusho aliyeitwa Jacques Sauniere Profesa msomi wa Harvard na mwandishi mzuri wa maandiko ya siri wa Ufaransa wanapewa kazi ya kufumbua ujumbe ulioachwa na mtunza nyumba ya makumbusho kabla ya kifo chake. Ujumbe unafunuliwa kuweka wazi hila kubwa katika historia ya wanadamu; kufichwa kwa ujumbe wa kweli wa Yesu Kristo na mamlaka ya siri ya Kanisa Katoliki la Roma iliyoitwa Opus Dei.
Kabla ya kifo chake, mtunza makumbusho alikuwa na ushahidi ambao ungeweza kukanusha utakatifu wa Kristo. Japokuwa (kulingana na hila) kanisa limejaribu kwa karne kuzima ushahidi, wafikiriaji wakubwa na wasanii wamepandikiza siri kila mahali: katika michoro kama vile Mona Lisa na Karamu ya Mwisho na Da Vinci, katika majengo ya makanisa, hata katika katuni za Disney. Madai makubwa ya kitabu ni haya:
- Mtawala wa Kirumi Constantini alishiriki kumfanya Yesu Kristo kuwa Mungu.
- Constantini binafsi alichagua vitabu vya Agano Jipya.
- Injili za Kiroho zilikatazwa na wanaume kuwakandamiza wanawake.
- Yesu na Maria Magdalena walioana kwa siri na walikuwa na mtoto.
- Maelfu ya nyaraka za siri zinakanusha hoja muhimu za Ukristu.
Brown aweka wazi hila zake kupitia mtaalamu wa vitabu vya kutunga, mwanahistoria wa koo za kifalme wa Uingereza Sir Leigh Teabing. Akidhihirishwa kama msomi mwenye busara wa kale, Teabing anaweka wazi kwa mwandishi-visiri (maandiko ya siri) Sophie Neveu kwamba katika Halmashauri ya Nicaea a.d. 325 “vipengele vingi vya ukristu vilijadiliwa na kupigiwa kura” kikiwemo cha utakatifu wa Yesu.
“Hadi wakati huo katika historia,” anasema “Yesu alionekana na wafuasi wake kama mtume mkuu… mtu mkuu mwenye nguvu, lakini ni mwenye nguvu licha ya kuwa binadamu”
Neveu anashtushwa. “Si Mwana wa Mungu?” anauliza.Teabing anaeleza: “Madai ya Yesu kama ‘Mwana wa Mungu’ yalipendekezwa rasmi na kupigiwa kura na Halmashauri ya Nicaea.”
“Subiri. Unasema utakatifu wa Yesu ulikuwa ni matokeo ya kura?”
“Kura ya karibu katika” Teabing anamweleza mwandishi visiri aliyeshangazwa.”[2]
Kwa hiyo, kulingana na Teabing, Yesu hakuchukuliwa kama Mungu hadi Halmashauri ya Nicaea kipindi cha a.d. 325, je ni lini kumbukumbu halisi za Yesu zinasadikiwa kupigwa marufuku au ziliharibiwa?
Hivyo, kulingana na nadharia, msingi mzima wa Ukristu umewekwa kwenye uongo. Siri za Da Vinci zimeuza hadithi yake vizuri, zikivuta mapendekezo toka kwa wasomaji kama vile “Ikiwa haikuwa kweli, isingechapishwa!” Mwingine alisema “hangetia mguu kanisani tena.” “Mrejea wa Kitabu alikisifu kwa utafiti wake makini kamilifu usio na dosari.”[3] Ushawishi mzuri kwa kazi kutunga.