Njia Ya Mitume
Ushahidi gani upo kwamba Yesu ni yule ambaye kweli alidai kuwa? Jinsi gani tunajua, hakuwa aina fulani ya mbabaishaji feki? Hebu tuangalie baadhi ya wababaishaji feki maarufu na tuone iwapo sifa hiyo inamfaa Yesu, au kwamba kuna ushahidi kuunga mkono madai yake.
Ferdinand Waldo Demara, mdogo, aliitwa mbabaishaji feki mkubwa. Demara alikuwa na utambulisho feki bandia wa mwanasaikolojia, mhadhiri wa chuo kikuu, mkuu wa idara ya chuo, na mkuu wa gereza. Alifanya hata upasuaji, akiwa kama daktari bogasi feki.
Baadhi wanadai kwamba Frank Abagnale alikuwa pia mbabaishaji feki mkubwa. Kati ya miaka 16 na 21, Abagnale alikuwa ni mmoja wa wasanii matapeli wenye mafanikio zaidi duniani. Aliwakabidhi cheki bandia za dola milioni mbili na nusu (2.5) katika nchi zote 50 na nchi 26 za kigeni.. Pia alifanikiwa kujifaulisha mwenyewe kama rubani wa ndege, mwanasheria, profesa wa chuo na mtaalamu wa magonjwa ya watoto kabla hajakamatwa na Polisi wa Ufaransa..
Ikiwa hadithi hii inaonekana kufahamika kwako, inawezekana ni kwa sababu ulitazama sinema ya mwaka 2002 Nikamate Kama Unaweza, ambamo Abagnale aliigizwa na Leonardo DiCaprio (ambaye alijipasisha mwenyewe kama mwingizaji katika Titanic).
Kitu gani kingefaa kushinda uigizaji wa Abagnale kama mtu tapeli? Haya, ikiwa Yesu Kristo hakuwa Masiha aliyedai kuwa, kungekuwa hakuna shindano. Hatuzungumzii kuhusu maelfu ya wanaotapeli, kama katika kesi ya Abagnale. Ikiwa Yesu Kristo alikuwa tapeli mbabaishaji feki, kazi yake ya utapeli ilidanganya mabilioni ya watu na ilibadilisha mwenendo wa miaka 2000 ya historia.
Hivyo Yesu angeweza kuwa Masiha feki, akidanganya hata wasomi wa kidini wakubwa? Inawezekana aliandaliwa na wazazi wake au wakufunzi wasiojulikana ili kuwa mfalme aliyeahidiwa muda mrefu ambaye Israel ilikuwa inamtafuta?
Kwa kweli, ikiwa Yesu alikuwa mbabaishaji feki, asingekuwa mtu wa kwanza katika historia ya Israel kuwa amedanganya kuhusu kuwa Masiha. Kupita karne zote kabla ya kuzaliwa Kristo, na baadaye pia, masiha wengi waliojitangaza wenyewe walitokea kuonekana kama matapeli na wendawazimu.
Tabiri za waebrania wa kale zilitabiri wazi utawala wa mfalme ajaye ambaye angeleta amani kwa Israel na kuwa mkombozi wao. Hali ya matarajio yaliijaza nchi na yalishika matumaini na matarajio ya wayahudi. Katika mazingira hayo kama ya waisraeli, ingewezekana mtu ambaye ana sifa kidogo, awekwe, au ajifananishe mwenyewe kufaa umbile la Masiha? Jibu kwa swali hilo limebaki katika Tabiri za Agano la Kale zikimwonyesha Masiha.
Kauli ya Mungu
Kulingana na maandiko, Mungu wa waebrania alizungumza kwa watu wake kupitia mitume, wanaume na wanawake ambao walikuwa wamezoezwa kwa Mungu ambaye angekuwa au asingekuwa sehemu ya uanzishaji wa kidini. Baadhi ya meseji za watume zilikuwa kwa wakati huu sasa, wengine kwa wakati ujao. Kwa vyovyote vile, kazi yao ilikuwa kutangaza matangazo ya Mungu na kujidhihirisha kwake kwa watu.
Kwa ujumla, kuwa mtume kulikuwa kama pamoja na kufanya kazi katika kiwanda cha kupaki nyama kati ya kazi za hatari zaidi duniani. Hata kama walikuwa wakisema kweli, mitume wangeweza kuuawa au kutupwa gerezani na watu waliokuwa hawapendi kile walichokuwa wanasema. (Baadhi ya wafalme walichukia kusikia habari mbaya.) Kulingana na maelezo ya kihistoria, mtume Isaya alikatwa nusu.
Hivyo fikiria mkanganyiko wa mtume: kifo ikiwa alithibitishwa kuwa sio sahihi na uwezekano wa kifo ikiwa alikuwa sahihi. Hakuna mtume wa kweli aliyetaka kumkosea Mungu, na wachache walitaka kukatwa nusu, katikati kwa msumeno. Hivyo mitume wengi walisubiri hadi walipoaminishwa kabisa kwamba Mungu amesema, au vinginevyo walifunga midomo yao. Wafalme walianza kutetemeka kwa hofu au ghadhabu. Ujumbe wa mtume wa kweli haukuwa sio sahihi.
Sasa hapa kuna swali: jinsi gani usahihi wa hawa mitume wa Biblia unalingana na watabiri wa leo.
Mitume kulinganisha na Watabiri?
Kupima kwamba usahihi wa watabiri wa kisasa unakaribia ule wa mitume wa Biblia, tumchukue Jean Dixon kama mfano halisi wa kujifunzia. Mtabiri huyu wa Kimarekani anaonekana kuwa na uwezo maalumu wa kutabiri mambo. Lakini kwenye uchambuzi sifa yake inaonekana haijathibitika.
Kwa mfano, Dixon alikuwa na maono kwamba mwezi Februari tarehe 5, 1962, mtoto alizaliwa Mashariki ya Kati ambaye angeibadili dunia kabla ya mwaka 2000. Huyu mtu maalumu angeunda dini ya dunia moja na kuleta amani ya dunia ya kudumu. Alikuwa ni msalaba unaokuwa juu ya mtu huyu hadi ufunike dunia nzima. Kulingana na Dixon, mtoto huyu angekuwa ni uzao wa malkia wa zamani wa Misri Nefertiti.[1] Yuko wapi jamaa huyu? Umemwona? Na vipi kuhusu hiyo amani ya dunia idumuyo – ni nzuri, eeh?
Kwa kweli, utafutaji mkubwa wa tabiri zake unatoa habari mbili zisizopingwa. Kiasi chake cha usahihi ni sawa na hao wanaokisia siku zijazo, na kutangaza zaidi kwa kutimia kwake kama tabiri zinavyokusudia kukisia idadi yoyote ya matukio yanayotokea kuwa ndiyo kutimia huko. Hata tabiri zilizotangazwa sana za Nostradamus zimekuwa mara nyingi zikithibitishwa kuwa sio sahihi licha ya madai yake yasiyo na uhakika, ambayo ni vigumu kuyakana kudai ni uongo.[2] Kwa mfano, hapa kuna moja ya tabiri za Nostradamus:
“Inahitaji Mungu-mke wa mbalamwezi, kwa siku yake na kutembea kwake: mzururaji na shahidi wa sheria ya Mungu, katika kuamsha maeneo makubwa ya ulimwengu kwenda kwa nia ya Mungu.”[3]
Hii inasemekana kuwa kuhusu kifo cha Binti Mfalme Diana. (Ulikuwa unafikiri inawezekana ni Margaret Thatcher.) Tabiri kama hii haziko wazi; ni kama kuona kitu katika mawingu. Lakini baadhi wanasisitiza huu ni ushahidi wa utabiri wa Nostradamus umetimizwa. Unafikiriwa sana, lakini ni vigumu kupinga kudai ni uongo.
Na hii ndiyo rekodi hasa ya mwenendo wa watabiri. Wakati “Kitabu cha Watu” kilipofanyia utafiti wa tabiri za watabiri 25 wa juu, asilimia 92 ya tabiri zilithibitishwa kuwa sio sahihi. Asimilia 8 zingine zilihojiwa na zingeweza kuelezewa kwa bahati au elimu ya jumla ya mazingira. [4] Katika majaribio mengine ya watabiri wa dunia maarufu wa kwanza, kiasi chao cha usahihi kimeonyeshwa kupita asilimia 11, ambayo inaweza kuwa sio wastani mbaya isipokuwa kwa ukweli kwamba watu wafanyao kukisia kwa haraka haraka kuhusu siku zijazo wanafikia katika asilimia ile ile. Hii haipingi kuelezea kote kwa siku zijazo, lakini kwa uhakika inaelezea kwanini watabiri hawashindi bahati nasibu.
Tofauti kati ya watabiri na mitume inaonekana kuwa zaidi ya aina moja kuliko aina ya digrii. Mitume walifanya matangazo maalumu kuhusu matukio ya siku zijazo kuhusiana na mpango wa Mungu unaonea toka katika hali madhubuti na walifanya hivyo kwa usahihi usioyumba. Watabiri ni zaidi ya mamluki, wanaotoa maelezo yasiyo hakika ya siku zijazo kwa soko lililo tayari kulipia huduma zao. Wanatoa taarifa za udadisi, lakini na rekodi yenye makosa.
Utabiri wa Kidini katika Mtazamo
Utabiri unaweza kuwa mafumbo kumshirikisha Mungu, wa kimantiki na kwa kukosa neno zuri, wa kutia hofu. Unaonesha picha za mahali na limwengu zingine. Katika Vita ya Nyota kuna utabiri wa moja itayoleta urari kwenye Nguvu. Sinema za Bwana wa Ulingo zinaweka hali zao za kufikirika katika mandhari za maneno ya kitabiri. Lakini hiyo ni dunia ya kufikirika.
Kuhusiana na dunia ya kweli, imesemekana kwamba ikiwa mtu angejua hata dakika moja ya wakati ujao angetawala dunia. Fikiria hilo. Kila dakika ya kujua kila mkono uliochangwa katika Kasino ya Kupiku. Ungekuwa mtu tajiri zaidi duniani na Donald angekuwa mtumishi wa Posta.
Lakini katika ulimwengu wa dini, utabiri unasaidia kazi muhimu. Inakuwa njia moja ya uhakika kujua ikiwa mtu anazungumza toka kwa Mungu au sio, kwa kuwa Mungu ajuaye yote angeweza kujua wakati ujao barabara. Na kwa hoja hii utabiri katika Agano la Kale unabaki kuwa wa kipekee, kwa kuwa vingi kati ya vitabu vitakatifu toka katika deni zingine hazina utabiri unaobashirika. Kwa mfano, wakati Kitabu cha Nabii Mormon na Hindu Veda vinadai maongozi matakatifu, hakuna namna kuthibitisha madai yao; unaachwa tu ukihisi “Ndio, hicho ni kama kitu ambacho Mungu angeweza kusema.
Msomi wa Biblia Wilbur Smith alilinganisha tabiri za Biblia na vitabu vingine vya kihistoria, akisema kwamba Biblia ni “mkusanyiko pekee uliotengenezwa na binadamu, au kundi la watu, ambamo ndani yake kunapatikana mkusanyiko mkubwa wa tabiri kuhusiana na taifa moja moja, Israel, watu wote wa dunia, miji fulani, na kuja kwa mmoja ambaye angekuwa Masiha.”[5] Hivyo, Biblia inaweka wazi maelezo yake kwa kuongoza katika namna ambayo inaweza aidha kuthibitishwa au kukanushwa.
Na ukiweka kiwango cha usahihi katika mtazamo wa kila siku, unaweza kuona jinsi gani inavyoshangaza. Kwa mfano, ingekuwa ajabu ikiwa mwaka 1910 ulitabiri kwamba mtu aitwaye George Bush angeshinda uchaguzi wa mwaka 2000. Lakini fikiria ungeweka baadhi ya haya maelezo katika utabiri wako:
- Mgombea mwenye karibu kura zote jumla angeshindwa uchaguzi.
- Mitandao yote ya Televisheni ingetangaza mshindi na kisha kugeuka.
- Nchi moja (Florida) ingeongoza uchaguzi.
- Mahakama Kuu ya Marekani mwishowe ikaamua mshindi.
Ikiwa hivyo ingetokea, kungekuwa na makanisa yaliyopewa majina yako na midori kwenye deshibodi ingekuwa na sura yako. Lakini haukuweka, hivyo hakuna. Kama ilivyo vigumu (au haiwezekani) kama ambavyo ingekuwa mwaka 1910 kuwa imetabiriwa kwa usahihi mlolongo sahihi wa matukio, uwezekano wa mambo kuwa hivyo ungekuwa mgumu kwa Yesu, au mtu yeyote kuwa ametimiza tabiri zote za waebrania kwa ajili ya Masiha. Zilizowekwa ndani ya Agano la Kale, zilizoandikwa mamia ya miaka kabla ya kuzaliwa kwa Yesu, ni tabiri mahususi 61 na karibu kumbukumbu 300 kuhusu Masiha.[6]
Kulingana na mahitaji ya waebrania kwamba utabiri lazima uwe na asilimia 100 kiwango cha usahihi, Masiha wa kweli wa Israeli lazima atimize yote au vinginevyo si Masiha. Kwa hiyo swali kwamba aidha inamthibitisha au inamfanya astahili kulaumiwa kwa udanganyifu mkubwa duniani?
Wezekano ni zipi?
Hebu tuangalie tabiri mbili maalumu kuhusu Masiha katika Agano la Kale.
“Wewe, O Bethlehem Ephrathah, ni kijiji kidogo tu nchini Yuda. Lakini bado mtawala wa Israeli atakuja toka kwako, mmoja ambaye asili zake ni kutoka nyakati za zamani za mbali.” (Mika 5:2, NLT)
“BWANA mwenyewe atachagua ishara. Angalia! Bikira atapata mtoto! Atazaa mtoto mwanamume na atamwita Immanueli – Mungu pamoja nasi.'” (Isaya 7:14, NLT)
Sasa, kabla ya kufikiria tabiri zingine 59, usimame na ujiulize watu wangapi katika aina ya Masiha watarajiwa katika historia yote walizaliwa na bikira katika mji wa Bethlehem. “Haya, hebu tuone, kuna jirani yangu George, lakini…. hapana, ngoja; alizaliwa Brooklyn.” Katika suala la tabiri 61 zilielezewa kwa kina kutimizwa na mtu mmoja, tunazungumzia hasa kuhusu nafasi zisizowezekana.
Wakati wanasayansi stadi walipogundua mlinganisho wa muundo wa DNA, wezekano za kuwa na mtu ambaye siye mara nyingi ni chini ya moja katika bilioni kadhaa (kitu kwa wapotoshaji kuweka akilini). Ingeonekana tuko kati mazingira yale yale jirani ya wezekano na sifuri, katika kufikiria mtu mmoja kutimiza tabiri hizi.
Profesa wa hisabati Peter Stoner aliwapa wanafunzi 600 swali la hisabati la uwezekano ambalo lingeng’amua uwezekano kwa mtu mmoja kutimiza tabiri nane maalumu. (Hii sio kama kurusha sarafu mara nane katika mlolongo na kupata kichwa kila mara.) Kwanza wanafunzi walikokotoa wezekano za mtu mmoja kutimiza masharti yote ya utabiri mmoja maalum, kama vile kusalitiwa na rafiki kwa vipande 30 vya fedha. Kisha wanafunzi walifanya vizuri zaidi kukadiria wezekano kwa tabiri zote nane kwa pamoja.
Wanafunzi walikokotoa kwamba wezekano kwa mtu mmoja kutimiza tabiri nane zote ni za kinyota- moja kwa kumi kwa kipeo cha 21.(1021). Kuelezea hiyo idadi, Stoner alitoa mfano ufuatao: “Kwanza, funika ardhi ya Dunia nzima kwa dola za fedha urefu wa futi 120. Pili, kwa madhumuni maalum, wekea alama mojawapo ya dola hizo na ifukie haraka haraka bila umakini. Tatu, mwambie mtu asafiri dunia nzima na kuchagua dola iliyowekewa alama huku akiwa amefungwa macho – haoni, kutoka katika trililioni za dola zingine”[7]
Watu wanaweza kufanya vitu vizuri na namba (hasa na jina la mwisho kama hilo), hivyo ni muhimu kufahamu kwamba kazi ya Stoner ilikaguliwa na Chama cha Kisayansi cha Marekani, ambacho kilisema, “Uchambuzi wa kihisabati…umewekwa kwenye kanuni za uwezekano ambazo zote zina maana na Profesa Stoner ametumia kanuni hizi katika njia ya ifaayo na namna inayoridhisha.”[8]
Pamoja na hiyo kama utangulizi, tuongeze tabiri sita zaidi kwa hizo mbili tulizofikiria tayari ili itupe jumla ya nane za Profesa Stoner:
Utabiri: Masiha angekuwa kutoka uzao wa Mfalme Daudi.Yeremia 23:5600 B.C. | Kutimia: “Yesu …mwana wa Daudi…”Luka 3:23, 314 B.C. | |
Utabiri: Masiha angesalitiwa kwa vipande 30 vya fedha.Zakaria 11:13487 B.C. | Kutimia: “Walimpa vipande thelathini vya fedha.”Mathayo 26:1530 A.D. | |
Utabiri: Masiha angetobolewa mikono na miguu yake.Zaburi 22:161000 B.C. | Kutimia: “Walikuja sehemu iliyoitwa Golgotha. Wote watatu walisulubishwa pale – Yesu kwenye msalaba wa katikati, na wahalifu wawili kila upande.”Luka 23:3330 A.D. | |
Utabiri Watu wangepiga kura kwa ajili ya vazi la Masiha.Zaburi 22:181000 B.C. | Kutimia “Askari… walichukua vazi lake, lakini lilikuwa halina mshono, limefumwa katika muundo mmoja kuanzia juu. Hivyo wakasema, ‘Tusilichane bali turushe daisi kuona nani analipata.'”Yohana 19:23-2430 A.D. | |
Utabiri: Masiha angeonekana akiendesha punda.Zakaria 9:9500 B.C. | Kutimia “Walileta wanyama wao kwake na wakatandika mavazi juu ya farasi wadogo, akakaa juu yake.”Mathayo 21:730 A.D. | |
Kutabiri: Mjumbe angetumwa kwenda kumsalimu Masiha.Malaki 3:1500 B.C. | Kutimia: Yohana akawaambia, “Ninabatiza kwa maji, lakini pale katika kundi la watu kuna mtu hamumjui.”Yohana 1:2627 A.D. |
Tabiri nane tulizorejea kuhusu Masiha ziliandikwa na watu kutoka nyakati na mahali tofauti kati ya miaka 500 na 1,000 kabla Yesu hajazaliwa. Hivyo hakukuwa na nafasi ya kula njama miongoni mwao. Angalia pia, mpangilio maalum. Hii si aina ya utabiri wa Nostradamus – “Ambapo mwezi unakuwa kijani, harage la lima linalala likifunikwa kando ya barabara.”
Nje ya Uwezo wake
Fikiria kushinda bahati nasibu ya Powerball yenye tiketi moja tu miongoni mwa milioni zilizouzwa. Hebu sasa fikiria kushinda mamia ya bahati nasibu hizi katika mlolongo. Watu wangefikiria nini? Kabisa, “Ilipangwa!”
Na zaidi ya miaka mitatu dai kama hilo limefanywa na wakosoaji kuhusu utimizaji wa utabiri wa Agano wa Kale. Wamekubali kwamba ni kweli Yesu alitimiza utabiri wa kimasiha lakini wamemshtaki kwa kuishi maisha yake katika namna ambayo ya kutimiza utabiri kwa makusudi. Ubishi mzuri lakini si wa kukubalika kama inavyoweza kuonekana.
Angalia sifa za tabiri nne za kimasiha:
- Uzao wake ungetokea kwa Daudi (Yeremia 23:5).
- Kuzaliwa kwake kungetokea Bethlehem (Mika 5:2).
- Angehamia Misri (Hosea 11:1).
- Angeishi Nazareth (Isaya 11:1).[9]
Sasa, kitu gani Yesu angefanya kuhusu kutimiza tabiri hizi? Si yeye wala wazazi walikuwa na udhibiti wa uzao wake. Kuzaliwa kwake Bethlehem kulikuwa ni matokeo ya sensa iliyoamriwa na Kaizari Agusto. Kuhamia kwa wazazi wake Misri kulisababishwa na utesaji wa Mfalme Herod. Na mara Herod alipokufa, wazazi wa Yesu waliamua kuishi Nazareth.
Hata katika umri mdogo msanii Yesu aliangalia katika tabiri alizokuwa nazo kwa bahati alitimiza na aliamua kuzifuata na kuona kama angeweza kutimiza zilizobaki, (kama mtu fulani anavyoamua kulenga kimwezi kwenye mchezo wa karata wa Hearts), rundo la karata bado lingepangwa dhidi yake. Angalia baadhi ya sababu katika tabiri tulizokwisha angalia: Masiha angesalitiwa kwa vipande thelathini vya fedha; angeuawa kwa njia ya kusulubiswa; na watu wangepiga kura kwa ajili ya nguo zake. Hizi tabiri zote zikawa kweli kwa Yesu, lakini ni nguvu gani aliyokuwa juu ya utimizaji wa yoyote kati ya hizi?
Wasomi wa Biblia wanatuambia kwa karibu kumbukumbu 300 kwa tabiri maalum 61 za Masiha zilitimizwa na Yesu Kristo. Nafasi za wezekano kwa mtu mmoja kutimiza hizo tabiri nyingi ingekuwa ni zaidi ya uwezekano wa kihisabati. Isingeweza kutokea, hata muda kiasi gani ungetolewa. Kadirio moja la wanahisabati la hizo nafasi zisizowezekana ni “nafasi moja kati ya trilioni, trilioni, trilioni, trilioni, trilioni, trilioni, trilioni, trilioni, trillion, trilioni, trilioni, trilioni, trilioni.”[10]
Bertrand Russell, mtu mbishi asiyeamini Mungu yupo, aliulizwa katika mahojiano ya gazeti la Look, ushahidi gani ungetolewa kwake ili yeye aamini Mungu. Russell alijibu, “OK, ningesikia sauti toka angani na ikatabiri mfululizo wa vitu na vikatokea, kisha nahisi ningeweza kuamini kuna aina fulani ya kiumbe asiye wa kawaida”
Msomi wa Biblia Norman Geisler alijibu ubishi wa Russell. “Ningesema, ‘Mr Russell, kumekuwa na sauti toka mbinguni; imetabiri vitu vingi; na tumeviona bila ubishi vikitokea.'”[11] Geisler alikuwa akigusia ukweli kwamba kiumbe wa mbali nje ya dunia angeweza kutabiri matukio ya siku zijazo.
Uthibitisho katika gudulia
Tumeangalia katika ushahidi kwa ajili ya utimizaji wa Yesu wa tabiri za kimasiha kutoka katika kila pembe isipokuwa mmoja. Kuna nini ikiwa mwandishi wa historia mKristu ambaye alinakili maandiko ya Isaya na vitabu vingine vya Agano la kale alivibadilisha kuvifanya vifanane na maisha ya Yesu?
Hili ni swali wasomi wengi na wakosoaji wameuliza. Na inaonekana inawezekana, hata inakubalika kwa kuitazama mwanzoni. Ingetuzuia sisi kumfanya Yesu ni tapeli mdanganyifu, ambayo inaonekana haiwezi kuwa hivyo kwa kiasi kikubwa. Hivyo, jinsi gani tunajua kwamba vitabu vya kinabii vya Agano la Kale, kama vile Isaya, Daniel, na Mika viliandikwa mamia ya miaka kabla ya Kristo, kama ilivyoonekana? Na ikiwa viliandikwa, jinsi gani twajua waKristu hawakubadili maandishi baadaye?
Kwa miaka 1,900, wakosoaji wengi walishikilia sana wazo hilo, ikizingatiwa katika kusikowezekana kwa binadamu kutabiri kwa usahihi matukio ya siku zijazo. Lakini kisha kitu fulani kikatokea ambacho kilizima udadisi wote wa njama za siri. Kitu kilichoitwa Maandiko ya Bahari iliyokufa.
Nusu karne kurudi nyuma, kuonekana kwa Maandishi ya Bahari iliyokufa kuliwapatia wasomi wa Biblia nakala za vitabu vya Agano la kale ambavyo vilikuwa vya zamani kuliko vingine vinavyojulikana kuwapo. Majaribio makubwa yalithibitisha kwamba nyingi ya nakala hizi zilitengenezwa hata kabla ya Yesu Kristu hajaisha. Na kwa kweli yanafanana na maandishi ya Biblia tuliyokuwa tayari tunatumia.
Matokeo yake, hata wasomi ambao wanamkana Yesu kuwa Masiha wanakubali maandishi haya ya Agano la Kale kuwa yametangulia kuzaliwa kwake na hivyo kukubali kwamba tabiri kuhusu Masiha ziliwekwa ndani yake hazijabadilishwa ili kuendana na Yesu.
Ikiwa tabiri hizi zilitimizwa kwa usahihi kupitia maisha ya Yesu, inaonekana ni sahihi kustaajabu kwanini kila mmoja nchini Israeli hakuweza kuona hili. Lakini kama kusulubishwa kwake kunavyotoa ushahidi, si kila mmoja alikuona [kusulubishwa huko]. Kama mtume Yohana alivyosema kuhusu Yesu, “Hata katika ardhi yake mwenyewe na miongoni mwa watu wake, hakukubaliwa.” (Yohana 1:11, NLT). Kwanini?
Kwa kufikiria historia iliyoimarishwa ya Israeli, si vigumu kusoma katika maana ya Masiha wazo la mpigania uhuru wa kisiasa. Inaeleweka jinsi gani karne ya kwanza mtu wa kiyahudi angeweza kufikiri, jinsi gani Masiha angekuja na Israeli bado ikakandamizwa chini ya ukaliaji wa Kirumi?
Wakati Yesu alipotimiza tabiri za kimasiha, alifanya hivyo katika namna ambazo hakuna yeyote alikuwa akitarajia. Alitafuta mapinduzi ya kimaadili na kiroho, si ya kisiasa, akitimiza malengo yake kwa sadaka binafsi na huduma ya kinyenyekevu, akiponya na kufundisha. Wakati huo huo, Israeli ilikuwa ikitafuta Musa mwingine au Joshua ambaye angewaongoza katika ushindi kupata tena himaya yao iliyopotea.
Bila shaka, wengi wa wayahudi kipindi cha Yesu walimtambua yeye kama Masiha – msingi mzima wa kanisa la kikristo ukiwa wa kiyahudi. Wengi wao, hata hivyo, hawakumtambua. Na si vigumu sana kuelewa kwanini.
Kuelewa vizuri matatizo kwa wayahudi karne ya kwanza, angalia huu utabiri wa kimasiha ulioandikwa miaka 700 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu na mtume Isaya. Ilikuwa inamzungumzia Yesu?
“Sisi sote tumepotea mbali kama kondoo. Tumeacha njia za Mungu kufuata zetu wenyewe. Lakini bado Bwana aliweka kwake hatia na dhambi zetu sisi sote”
“Aliteswa na kutendewa kikatili, lakini hakusema neno. Aliongozwa kama mwanakondoo kwenda machinjioni. Na kama kondoo alivyo kimya mbele ya mkata manyoya, hakufungua mdomo wake. Tokea gerezani na katika mashitaka walimpeleka mbali kwenye kifo chake. Lakini nani miongoni mwa watu alitambua kwamba alikuwa akifa kwa ajili ya dhambi zao na kwamba alikuwa akiteseka kwa adhabu yao? Hakufanya kosa, na hakuwahi kumdanganya yeyote. Lakini alizikwa kama mhalifu; aliweka kwenye kaburi la mtu tajiri.”
“Lakini ilikuwa mpango mzuri wa Bwana kumnyong’onyesha na kumjaza huzuni. Lakini wakati maisha yake yanafanywa sadaka kwa ajili ya dhambi, atakuwa na umati wa watoto, warithi wengi. …Na kwa sababu ya kile alichokiona, mtumishi wangu mwenye haki atafanya iwezekane wengi kuhesabiwa wenye haki, kwa sababu atabeba dhambi zao zote.” (Sehemu za Isaya 53:6-11, NLT)
Wakati Yesu alipokuwa akining’inia msalabani, baadhi kama inavyoeleweka wamekuwa wakifikiri, “Jinsi gani huyu anaweza kuwa Masiha? Kwa wakati ule ule, wengine huenda wamekuwa wakishangaa, “Nani mwingine kama si Yesu Isaya angekuwa anamzunguzia?’
Mbabaishaji tapeli asiyewezekana
Hivyo ni kitu gani tufanye kuhusu Yesu kutimiza tabiri nyingi sana zilizoandikwa mamia ya miaka kabla ya kuzaliwa kwake? Leonardo DiCaprio … Ninamaanisha, Frank Abagnale anaweza kuwa msanii mbabaishaji mzuri, lakini alikamatwa kipindi alipokuwa mzee kiasi cha kunywa bia kihalali.
Yesu haonekani kama alivyo mtaalamu Frank Abagnale. Yuko katika aina tofauti kabisa. Hakuna mbabaishaji angeweza kushinda nafasi hizo kama zile zilizowasilishwa na utabiri wa kiebrania.
Na hiyi inamaanisha nini? Hitimisho mbizi zinajitokeza: Kwanza, ni kiumbe cha mbali kingeweza kuelekeza matukio haya. Na pili, inafanya madai yote mengine ya Yesu yawe na maana na thamani ya kuangaliwa kwa dhati.
Katika Injili ya Yohana, Yesu alifanya dai, “Mimi ni njia, ukweli na uzima.” Ushahidi mzito unaonekana kuonesha kwamba uthibitishaji katika habari hiyo si wa kugushi.
Je, ni kweli Yesu alifufka toka katika Wafu?
Swali kubwa zaidi la wakati wetu “Nani ni Yesu Kristo wa kweli?” Alikuwa tu mtu wa pekee, au alikuwa Mungu katika mwili, kama Paulo, Yohana na wafuasi wake waliomini?
Mashahidi wa macho kwa Yesu Kristo kwa kweli walizungumza na walitenda kama walivyoamini, aliinuka kimwili toka katika wafu baada ya kusulubiwa kwake. Ikiwa hawakuwa sahihi basi Ukristu umejengwa katika uongo. Lakini kama walikuwa sahihi, muujiza huo ungethibitisha yote Yesu alisema kuhusu Mungu, yeye mwenyewe na sisi.
Lakini lazima tuchukue ufufuko wa Yesu Kristo kwa imani pekee, au kuna ushahidi mzito wa kihistoria? Wakosoaji wachache walianza uchunguzi kwenye rekodi za kihistoria kuthibitisha maelezo ya ufufuko ni uongo. Ni kitu gani waligundua?
Je, Yesu alisema kitu gani kinatokea baada ya sisi kufa?
Ikiwa ni kweli Yesu alifufuka toka katika Wafu, basi lazima ajue kitu gani kipo upande mwingine. Ni kitu gani alisema kuhusu maana ya maisha na siku zetu zijazo? Kuna njia nyingi kwenda kwa Mungu au Yesu alidai kuwa njia pekee? Soma majibu ya kushangaza “Kwanini Yesu?”
Bonyeza hapa kusoma “Kwanini Yesu?” na gundua kile Yesu alisema kihusucho maisha baada ya kifo.
Ni kweli Yesu alifufuka toka katika Wafu?
Mashahidi wa macho kwa Yesu Kristo kwa kweli walizungumza na walitenda kama walivyoamini, alifufuka toka katika wafu baada ya kusulubiwa kwake. Ikiwa walikosea basi uKristu umeanzishwa kwa uongo? Lakini kama walikuwa sahihi, muujiza huo ungethibitisha yote Yesu aliyosema kuhusu Mungu, kuhusu yeye na kutuhusu sisi.
Lakini ni lazima tuamini ufufuko wa Yesu Kristo kwa imani pekee, au kuna ushahidi wowote wa kihistoria? Wakosoaji kadhaa walianza uchunguzi kwenye kumbukumbu za kihistoria kujaribu kuona kama kweli maelezo ya ufufuko yalikuwa uongo. Kitu gani waligundua?
Kuangalia ushuhuda wa madai makuu yaliyowahi kufanyika ya ufufuko wa Yesu Kristo!
Bonyeza hapa kwa ajili ya kudai zaidi fantastic milele alifanya – ya ufufuo wa Yesu Kristo!