Wasifu Uliozaliwa
Yesu Kristo kweli alikuwapo, au Ukristu umejengwa kwa uzushi? Wasomi wachache wanahoji kuwapo kwa Yesu, lakini baadhi ya maadui wa ukristu wanajaribu kuthibitisha vinginevyo.
Katika shitaka dhidi ya Vatican, Kanisa lilishitakiwa kwa kubuni uzushi wa kuwapo kwa Yesu. Ingawaje kesi ilitupiliwa nje ya Mahakama mwezi Februari 2006, mdai, Luigi Cascioli, alikata rufaa, lakini mwishowe kesi yake ilifungwa.
Madai dhidi ya uwapo wa Yesu yaliwekwa wazi kwenye Televisheni ya CNN wakati Ellen Johnson, raisi wa wasioamini kuwapo kwa Mungu wa Marekani, walipotangaza:
“Ukweli ni kwamba hakuna hata chembe ya ushahidi wa kawaida kuwa kulikuwapo na Yesu Kristo. Yesu Kristo na Ukristu ni dini ya siku hizi. Na Yesu Kristo ni mkusanyo toka miungu mingine: Osiris, Mithras, aliyekuwa na asili ile ile, kifo kile kile kama cha kiimani cha Yesu Kristo.” Ellen Johnson, mpagani
Johnson na baraza la utepe-bluu la viongozi wa kidini walikuwa wakijadili swali, “Kitu gani kinatokea baada sisi kufa?” kwenye kipindi cha moja kwa moja cha Larry King Live katika matangazo ya CNN. Mtangazaji King aliyetulia mara nyingi aliketi kwa makini na kisha akajibu.”Kwa hiyo hauamini kulikuwa na Yesu Kristo?
Kwa hali ya uhakika, Johnson alijibu, “Hakuwapo.” Si kile ninachoamini; hakuna ushahidi wa kawaida kwamba YK, Yesu Kristo alikuwapo.”
King hakufuatilia na alienda katizoni kwa Tangazo la Biashara. Hakuna mjadala wa ushahidi wowote kwa ajili au dhidi ya kuwapo kwa Yesu ulikuwa unakuja. Watazamaji wa kimataifa wa Televisheni waliachwa wakishangaa.[1]
Miaka hamsini mwanzoni, katika kitabu chakeKwanini mimi si mkristu, asiyeamini Mungu Bertrand Russell alishtusha watu wa kizazi chake kwa kuhoji kuwapo kwa Yesu. Aliandika:
“Kihistoria inatia shaka kwamba Kristo alikuwapo hata kidogo, na kama alikuwapo, hatujui kitu chochote kuhusu Yeye, hivyo sihusiki na suala la kihistoria, ambalo ni gumu sana.”[2]
Inawezekana kwamba Yesu wengi wanaomwamini hakuwahi kuwapo? Katika Hadithi ya Ustaarabu, mwanahistoria wa kawaida Will Durant alileta swali hili: “Yesu aliwahi kuwapo? Ni hadithi ya maisha ya mwasisi wa Ukristu, matokeo ya huzuni ya mwanadamu, fikira na matumaini – hadithi inayolingana na ya Krishna, Osiris, Attis, Adonis, Dionysus na Mithras?” [3] Durant alionesha jinsi gani hadithi ya ukristu ina mifanano mingi ya kutia shaka kwa hadithi za miungu ya kipagani.”[4]
Baadaye katika makala hii tutaona jinsi gani huyu mwanahistoria mkubwa alijibu swali lake mwenyewe kuhusu kuwapo kwa Yesu. Kwa hiyo, jinsi gani tunaweza kujua kwa uhakika kwamba mtu huyu, ambaye wengi wanamwabudu na wengine wanamlaani, alikuwapo kweli? Johnson yupo sawa wakati aliposema kwamba Yesu Kristo ni mkusanyiko toka kwa miungu wengine? Na Russell yuko sawa wakati aliposema kwamba kuwapo kwa Yesu ni “mashaka kabisa”?
Hadithi dhidi ya Ukweli
Ngoja tuanze na swali la msingi zaidi: Kitu gani kinatofautisha hadithi na ukweli? Jinsi gani tunajua, kwa mfano, kwamba Alexander Mkuu alikuwapo kweli? Inavyoaminika, katika mwaka 336 baada ya Kristo, Alexander Mkuu alikuwa mfalme wa Masedonia katika umri wa miaka 20.. Mwerevu wa jeshi, huyu kiongozi maridadi mwenye kiburi alichanja njia kupitia vijiji, miji na falme za Uajemi za Greco hadi akazitawala zote. Katika kipindi kifupi cha miaka minane majeshi ya Alexander yalivuka jumla ya maili 22,000 katika kuzishinda kwake na kuzitwaa nchi hizo.
Imekuwa ikisemwa kuwa Alexander alikuwa akilia wakati alipozikimbilia nchi za kuzishinda. (Ninafikiri huyu siye mtu ninayetaka kucheza naye.)
Kabla hajafa katika umri wa miaka 32, Alexander inavyoripotiwa alitimiza vitendo vikubwa vya jeshi kuliko yeyote katika historia, sio tu za wafalme walioishi kabla yake, lakini pia vya hao waliokuja baadaye, hadi katika wakati wetu. Lakini leo, mingineyo ya idadi ya miji iliyoitwa Alexandria, sinema inayochosha na Oliver Stone, na vitabu vichache, urithi wake wote umesahaulika. Kwa kweli jina Colin Farrell lina nguvu zaidi ya kuvutia katika ofisi ya sinema kuliko jina la Alexander.
Licha ya kushindwa kwa ofisi ya sinema, wanahistoria wanaamini Alexander alikuwapo kwa sababu ya sababu tatu za msingi:
- Nyaraka zilizoandikwa kutoka kwa wanahistoria wa zamani.
- Mchango wa kihistoria.
- Ushahidi wa kihistoria na kitafiti.
Nyaraka za Kihistoria Kuhusu Yesu
Historia ya Alexander Mkubwa na ushindi wake wa kijeshi unapatikana kutoka katika vyanzo vitano vya kale, hakuna hata kimojawapo kilikuwa na mashahidi wa macho. Ingawaje imeandikwa miaka 400 baada ya Alexander, Kitabu cha Plutarch Cha Maisha ya Alexander ni maelezo ya msingi ya maisha yake.
Kwa Bw. Plutarch and waandishi wengine waliondolewa miaka mia saba kutoka katika matukio ya maisha ya Alexander, walitegemeza taarifa zao katika maelezo ya mwanzo. Kati ya maelezo ishirini ya kihistoria ya wakati huo kuhusu Alexander, hakuna hata mojawapo linaendelea kuwapo. Maelezo ya baadaye yapo, lakini kila moja linamwelezea “Alexander” tofauti, kabisa na kufikiria kwetu. Lakini bila kujali pengo la muda la miaka saba, wanahistoria wanaaminishwa kwamba Alexander alikuwa ni mtu wa kweli na kwamba maelezo ya msingi ya kile tusomacho kuhusu maisha yake ni kweli.
Tukimweka Alexander kama hoja ya kukumbushia, tutatambua kwamba kwa Yesu kuna maelezo yote ya kidini na ya kihistoria ya kawaida. Lakini lazima tuulize swali, yaliandikwa na wanahistoria wa kuaminika wenye mwelekeo? Hebu tuangalie kwa kifupi.
Agano Jipya
Vitabu 27 vya Agano Jipya vinadaiwa kuandikwa na watunzi ambao aidha walimjua Yesu au walipokea ufahamu wake wa kwanza toka kwa wengine. Maelezo ya Injili nne zinarekodi maisha na maneno ya Yesu kutoka katika mitazamo tofauti. Maelezo haya yamechunguzwa kwa makini sana na wasomi wote wa Ukristu na nje yake.
Msomi John Dominic Crossan anaamini kwamba chini ya asimilia 20 ya kile tusomacho katika Injili ni maneno halisi ya Yesu. Hata huyu mkosoaji habishi kwamba Yesu Kristo kweli aliishi.
Licha ya maoni ya Crossan, na wale wasomi wachache wa upande mwingine kama Yeye, makubaliano ya wanahistoria wengi ni kwamba maelezo ya Injili yanatupa sisi picha nzuri ya Yesu Kristo. Iwe kwamba maelezo ya Agano Jipya ni ya kuaminiwa ni somo la makala nyingine (Angalia “Andiko la Yesu“), hivyo tutaangalia kwenye vyanzo vingine visivyo vya kikristu kwa jibu letu kwamba Yesu alikuwapo.
Maelezo ya Watu Wasio-Wakristu wa kale
Hivyo wanahistoria gani wa karne ya kwanza walioandika habari ya Yesu hawakuwa na agenda ya kikristu? Kwanza kabla ya yote, hebu tuangalie kwa hao maadui wa Yesu.
Wapinzani wake wa Kiyahudi walikuwa na mengi ya kufaidika kwa kukana kuwapo kwa Yesu. Lakini ushahidi unaonesha katika uelekeo mwingine. “Maandiko kadhaa ya Kiyahudi pia yanaelezea kuwapo kwa mwili na damu yake. Maandiko yote ya Gemara ya Kitabu cha Wayahudi; Talmud yanamtaja Yesu. Ingawaje haya yanajumuisha vifungu vichache vifupi vilivyokusudiwa kutohesabu utakatifu wa Yesu, maandiko haya ya kale ya Kiyahudi hayaanzi kusema kwamba hakuwa mtu wa kihistoria.”[5]
Flavius Josephus alitambulika kama mwanahistoria wa Kiyahudi aliyeanza kuandika chini ya Mamlaka ya Kirumi A.D. 67. Josephus, ambaye alizaliwa miaka michache baada ya Yesu kufa, angefahamu kwa kina zaidi sifa ya Yesu miongoni mwa Warumi na Wayahudi. Katika zile maarufu Nyakati za Wayahudi (A.D. 93), Josephus aliandika habari ya Yesu kuwa ni mtu kweli. “Katika wakati huo Yesu aliishi kama mtu mtakatifu, ikiwa mtu aliweza kupewa sifa hiyo, kwa kuwa alifanya kazi za ajabu, na alifundisha watu, na kwa furaha aliupokea ukweli. Na alifuatwa na wayahudi wengi na wagiriki wengi. Alikuwa ni Masiha.”[6] Ingawa kuna ubishi kuhusu baadhi ya maneno katika maelezo, hasa kumbukumbu kwa Yesu kuwa Masiha (wasomi wanahoji, wanafikiri kwamba wakristu waliingiza vineno hivi (kirai), kwa hakika Josephus alihakikisha kuwapo kwake.
Vipi kuhusu wanahistoria wa kawaida ambao waliishi katika nyakati za kale lakini hawakuchochewa kidini? Kuna uthibitisho uliopo wa waandishi angalau 19 wa kawaida wa kale ambao walitengeneza kumbukumbu za Yesu kuwa ni mtu wa kweli.[7]
Mmoja wa wanahistoria wakubwa kwa nyakati za kale, Cornelius Tacitus, alitangaza kwamba Yesu aliteseka chini ya Pilato. Tacitus alizaliwa karibu miaka 25 baada ya Jesu kufa, na alikwisha ona kuenea kwa Ukristu kukianza kuimeza Roma. Mwanahistoria wa Kirumi aliyeandika kinyume cha Kristo na Wakristo, akiwatambulisha mwaka A.D. 115 kama harakati za watu waliochukizwa kwa matendo yao maovu, na kwa kawaida waliitwa Chrestiani. Jina lilitolewa toka kwa Chretus, ambaye, katika utawala wa Tiberius, aliteswa chini ya Pontius Pilato, Wakili wa Yuda.”[8]
Habari hizi za kweli zinazofuata kuhusu Yesu ziliandikwa na vyanzo vya kale visivyo vya kikristu:
- Yesu alikuwa wa kutoka Nazareth.
- Yesu aliishi maisha ya busara na maadilifu.
- Yesu alisulubiwa nchini Yuda chini ya Pontio Pilato wakati wa utawala wa Tiberius Caesar wakati wa Pasaka, akidhaniwa kuwa ni Mfalme wa Wayahudi.
- Yesu aliaminiwa na wafuasi wake kuwa amekufa na amefufuka toka katika wafu siku tatu baadaye.
- Maadui wa Yesu walikubali kwamba alitenda mambo yasiyo ya kawaida waliyoiita “miujiza.”
- Kundi ndogo ya wafuasi wa Yesu liliongezeka haraka, likaenea mbali hadi Roma.
- Wafuasi wa Yesu walikataa miungu mingi, waliishi maisha maadilifu, na walimwabudu Kristo kama Mungu.
Mwanateolojia Norman Geisler aliandika:
“Maelezo haya ya jumla yanaendana kikamilifu na hayo ya Agano Jipya”[9]
Yote katika ya haya maelezo yasiyotegemeana, ya kidini na kawaida, yanazungumzia mtu wa kweli aliyelingana sawa na Yesu katika Injili. Encyclopedia Britannica inanukuu haya maenezo mbalimbali ya kawaida ya maisha ya Yesu kuwa ni ushahidi thibitifu wa kuwapo kwake. Inaeleza:
“Maelezo haya yasiyotegemeana yanathibitisha kwamba katika nyakazi za kale hata wapinzani wa Ukristu hawakutilia shaka uwekaji historia ya Yesu.”[10]
Mchango wa kihistoria
Tofauti muhimu kati ya uzushi na mtu wa kweli ni jinsi gani mtu anavyobadili historia. Kwa mfano, vitabu vimeandikwa na sinema zimetengenezwa kuhusu Mfalme Arthur wa Camelot na mashujaa wake wa meza ya duara. Wahusika hawa wamekuwa mahiri kiasi wengi wanaamini walikuwa watu kweli. Lakini wanahistoria wametafuta vyanzo kwa kuwapo kwao wameshindwa kugundua faida yoyote waliyo nayo kwenye sheria, maadili au dini. Himaya pamoja na ukuu wa Camelot kwa hakika ungeacha alama zake kwenye historia za wakati huo. Kukosekana huku kwa umuhimu wa kihistoria kunaonesha Mfalme Arthur na mashujaa wake wa meza ya duara ni wa kutunga tu.
Mwanahistoria Thomas Carlyle alisema, “Hakuna mtu mkuu anayeishi bure. Historia ya dunia ni habari ya watu wakuu.”[11] Kama Carlyle alivyonoti, ni watu wa kweli, sio hadithi, ambayo wanabadili historia.
Akiwa mtu kweli, Alexander alibadili historia kwa ushindi wa majeshi yake, alibadili mataifa, serikali na sheria. Lakini vipi kuhusu Kristo na mchango wake katika dunia yetu?
Serikali za karne ya kwanza za Yuda and Roma hazikuguswa kwa kiasi kikubwa na maisha ya Yesu. Mwananchi wa kawaida wa Rumi hakujua alikuwapo hadi miaka mingi baada ya kifo chake. Utamaduni wa kirumi ulibaki kwa kiasi kikubwa kimya na mbali na mafundisho yake kwa miongo kadhaa, na ingeweza kuwa karne kadhaa kabla ya kuua wakristu katika uwanja wa mauaji hakujawa starehe ya kupotezea muda ya kitaifa. Sehemu ya dunia iliyobaki ilikuwa nazo kidogo kama zilikuwapo taarifa zake. Yesu hakukusanya jeshi. Hakuandika kitabu wala kubadilisha sheria. Viongozi wa kiyahudi walitarajia kufuta kumbukumbu zake na ilionekana wangefanikiwa.
Leo, hata hivyo, Roma ya kale imelala katika magofu. Majeshi yenye nguvu ya Kaizari mfahari wa mamlaka ya kibeberu ya Rumi yamepotelea katika kusahauliwa. Lakini jinsi gani Yesu anakumbukwa leo? Ni nini huo wake mvuto unaoendelea?
- Vitabu vingi vimeandikiwa kuhusu Yesu kuliko mtu mwingine yeyote katika historia.
- Mataifa yametumia maneno yake kama kanuni za msingi katika serikali zao. Kulingana na Durant, “Shangwe ya Kristo ilikuwa ndio mwanzo ya demokrasia.”[12]
- Mafundisho yake katika mlima yaliweka mfano halisi mpya katika kanuni na maadili.
- Shule, hospitali na kazi za kibinadamu zimeanzishwa kwa jina lake. Harvard, Yale, Princeton, na Oxford ni vyuo vichache ambavyo vina wakristo wa kuwashukuru kwa kuanzishwa kwao.
- Faida zilizoheshimiwa za wanawake katika Utamaduni wa Magharibi zinaelekezea mizizi yake kwa Yesu. (Wanawake katika nyakati za Yesu walifikiriwa kuwa duni na si watu hadi mafundisho yake yalipofuatwa.)
- Utumwa ulikomeshwa nchini Uingereza na Marekani kutokana na mafundisho ya Yesu kwamba kila maisha ya binadamu yana thamani kuthaminika.
- Wategemezi wa zamani wa madawa ya kulevya na pombe, malaya na wengine watafutao maana katika maisha wanadai yeye kama kielelezo kwa ajili ya maisha yao yaliyobadilika.
- Watu bilioni mbili wanajiita wakristu. Wakati baadhi ni wakristu kwa jina tu, wengine wanaendelea kubadili utamaduni wetu kwa kufundisha maadili ya Yesu kwamba maisha yote ni yenye thamani ya kuthaminika na tunapaswa kupendana, kumpenda kila mmoja.
Kwa kushangaza, Yesu alifanya yote ya badiliko hili kama matokeo ya idara ya kazi ya kipindi cha miaka mitatu tu. Ikiwa Yesu hakuwapo, mtu lazima ashangae jinsi gani uzushi ungeweza kubadili historia hivyo. Wakati mwanahistoria wa dunia H.G. Wells alipoulizwa nani ameacha urithi mkubwa katika historia, alijibu, “kwa swali hili Yesu anashikilia nafasi ya kwanza.”[13]
Ushahidi wa kimaandishi na faida ya kihistoria unalenga kwenye ukweli kwamba Yesu alikuwapo. Ikiwa Yesu kweli alikuwapo, pia tungetarajia kugundua nyayo zake zilizowekwa ndani ya maelezo yake ya historia. Uzushi, huwa hauachi maelezo ya kuthibitisha hivi.
Moja ya siri hapa kwa Durant na wasomi wengine ni suala la muda. Uzushi na uvumi/hekaya kwa kawaida huchukua mamia ya miaka kuzuka – hadithi ya George Washington hakuwahi kusema uongo inawezekana ilikuwa uongo, hadi karne mbili zilipoibadili kuwa historia. Habari za Ukristu, kwa upande mwingine, zilienea kwa haraka kiasi cha kuhesabiwa kuwa uzushi. Ikiwa Yesu hakuishi, hao ambao wanapinga ukristu wangemwita mzushi tokea mwanzo. Lakini hawakuthubutu.
Ushahidi wa hivyo, sambamba na maelezo yaliondikiwa ya kale na mchango wa kihistoria wa Yesu Kristo, unawaaminisha hata wanahistoria wakosoaji kwamba mwasisi wa Ukristu hakuwa mzushi wala uvumi/hekaya. Lakini mtaalamu mmoja katika uzushi hakuwa na uhakika sana.
Kama Muggeridge, msomi wa Oxford C. S. Lewis mwanzo aliamini kwamba Yesu hakuwa kitu chochote zaidi ya kuwa mzushi. Lewis mwanzo alisema, “Dini zote, yaani imani zote… ni ubunifu tu mwanadamu mwenyewe – Kristo kama ilivyo sana kwa Loki.”[14] (Loki mungu za wa zamani wa Unorweini (Norway). Kama Thor, lakini bila mtindo wa nywele kuzifunga kwa nyuma.)
Miaka kumi baada ya kumkana Yesu kuwa ni uzushi, Lewis aligundua kwamba maelezo ya kihistoria, zikiwamo nyaraka kadhaa za mashahidi wa macho, zinathibitisha kuwapo kwake.
Yesu Kristo ameibadili sura ya historia kama tememeko kubwa la ardhi. Na tetemeko hili limeacha alama ya njia pana kuliko bonde kubwa. Ni alama-njia hii ya ushahidi ambao inawaaminisha wasomi kwamba Yesu kweli alikuwapo na kweli alibadili dunia yetu miaka 2000 iliyopita.
Mkosoaji mmoja ambaye alifikiri Yesu alikuwa mzushi alikuwa mwandishi wa habari wa Uingereza Malcolm Muggeridge. Lakini kwenye kipindi cha Televisheni kwa Israel, Muggeridge alikabiliwa na ushahidi kuhusu Yesu Kristo ambao hakujua ulikuwapo. Wakati akiangalia sehemu za kihistoria – Sehemu aliyozaliwa Yesu ya Bethlehem, mji wa Nazareth, eneo la kusulubishiwa, na kaburi tupu – hisia za Ukweli wa Yesu zilianza kujitokeza.
Baadaye alieleza:
“Ilikuwa ni wakati nilipokuwa katika Ardhi Takatifu kwa dhumuni la kufanya vipindi vitatu vya Televisheni vya BBC katika Agano Jipya kwamba uhalisia ulinishika kuhusu kuzaliwa kwa Yesu, idara yake na kusulubiwa. …Nikafahamu kwamba kulikuwa na mtu, Yesu, ambaye pia alikuwa Mungu.”[15]
Baadhi ya wasomi wajerumani wadadisi zaidi katika karne za 18 na 19 walihoji kuwapo kwa Yesu, wakizungumzia wahusika wakuu kama Pontio Pilato na kasisi mkuu Joseph Caiaphas katika maelezo ya Injili hawajahakikishwa kuwa kweli. Hakuna kanushi zilizowezekana hadi katikati ya karne ya 20.
Mwanaakilojia (mwana-elimu kale) katika mwaka 1962 alihakikisha kuwapo kwa Pilato wakati walipogundua jina lake likiwamo katika maandishi yaliyochongwa katika jiwe lililochimbwa. Vile vile, kuwapo kwa Caiaphas hakukuwa dhahiri hadi 1990, wakati kasha la mifupa lilipogunduliwa likiwa na maandishi yake yaliyochongwa. Wana-elimu kale (wana-akiolojia) pia wamegundua kile wanachoamini kuwa nyumba ya Simoni Petro and pango ambapo Yohana mbatizaji alipofanyia ubatizaji wake.
Mwishowe, labda ushahidi mwingine unaothibitisha zaidi kwamba Yesu alikuwapo ni mwongezeko kwa kasi wa ukristu. Jinsi gani inaweza kuelezwa bila Kristo? Jinsi gani hili kundi la wavuvi and wafanyakazi wengine walimfahamu Yesu ndani ya miaka michache? Durant alijibu swali lake mwenyewe la utangulizi – Yesu alikuwapo? —kwa hitimisho lifuatalo:
Kwamba watu wachache wa kawaida ndani ya kizazi kimoja wangefahamu wasifu wa mtu mwenye nguvu na kuvutia sana, mzito na mwenye maadili na anayeongoza maono ya udugu wa kibinadamu, ni muujiza ajabu zaidi kuliko yote katika Injili . Baada ya karne mbili za Ukosoaji Mkali, maelezo ya maisha, tabia na mafundisho ya Kristo yalibaki wazi kimsingi, na sura ya kupendeza katika historia ya mtu wa magharibi.
Uamuzi wa Wasomi
Clifford Herschel Moore, profesa katika Chuo Kikuu cha Harvard, alisema Uhakiki wa Historia ya Yesu, pia Ukristu ulimjua Mwokozi na Mkombozi wake sio kama baadhi ya miungu ambao historia zao ziliwekwa kwa imani za kizushi. …Yesu alikuwa ni wa kihistoria na si kiumbe cha kizushi. Hakuna uzushi wa mbali au wa kimakosa uliojiingiza kwa mwamini wa kikristu; imani yake ilianzishwa kwenye ukweli endelevu, wa kihistoria na unaokubalika”[16]
Ni wachache ikiwa wapo wanahistoria wa kweli wanakubaliana na Ellen Johnson na madai ya Berttrand Russell kwamba Yesu hakupata kuwapo. Uhakiki zaidi kumbukumbu za maisha ya Yesu na waandishi wa wakati huo, mchango wake mkuu kihistoria, na ushahidi wa kuhakikisha unaonekana umewashawishi wasomi kwamba Yesu kweli alikuwapo. Uzushi ungeweza kufanya yote hayo? Wote isipokuwa wakosoaji wachache wakali wanasema hapana.
Dr. Michael Grant wa Cambridge ameandika, “Kuweka pamoja, njia za kisasa za kidadisi zimeshindwa kukubaliana na dai la uzushi wa Kristo. Imejibiwa tena na tena na imeharibiwa kwa maneno na wasomi wa ngazi ya juu.’Katika miaka ya hivi karibuni hakuna msomi wa dhati amethubutu kudai kutohakikiwa historia ya Yesu.”[17]
Mwanahistoria ya Chuo cha Yale Jaroslav Pelikan alitangaza, “Bila kujali kile mtu yeyote anachoweza kufikiri binafsi au kuamini kuhusu Yeye, Yesu wa Nazareth amekuwa mhusika mkuu katika historia ya utamaduni wa magharibi kwa karibu karne ishirini. …Tangu kizazi chake kwamba mengi ya mataifa ya mwanadamu yanaweka kalenda yake kwa jina lake, mamilioni wanamlaani na pia katika jina lake mamilioni wengine wanasali.”[18]
Je ni kweli Yesu alifufuka toka katika Wafu?
Swali kubwa kabisa la wakati wetu “Nani ni Yesu Kristo kweli?” Alikuwa mtu tu wa pekee, au alikuwa Mungu katika mwili, kama Paulo, Yohana, na wafuasi wake walivyoamini? (Angalia “Yesu ni Mungu?“)
Mashahidi wa macho kwa Yesu Kristo kwa kweli walizungumza na walitenda kama walivyoamini, aliinuka kimwili toka katika wafu baada ya kusulubiwa kwake. Ikiwa hawakuwa sahihi basi Ukristu umejengwa katika uongo. Lakini kama walikuwa sahihi, muujiza huo ungethibitisha yote Yesu alisema kuhusu Mungu, yeye mwenyewe na sisi.
Lakini lazima tuchue ufufuko wa Yesu Kristo kwa imani pekee, au kuna ushahidi mzito wa kihistoria? Wakosoaji wachache walianza uchunguzi kwenye rekodi za kihistoria kuthibitisha maelezo ya ufufuko ni uongo. Ni kitu gani waligundua?
Kulikuwa na Hila za Da Vinci ?
“Mona Lisa’s Smirk” inachunguza dhana ya hila inayoongoza duniani kuhusu Yesu Kristo. Je, Yesu na Maria Magdalena waliooana? Je, Constantine aliamuru kuharibiwa kwa rekodi za kweli za Yesu Kristo na kutambua kuwa Mungu wakristu wanavyomwabudu leo?
Bonyeza hapa kugundua ukweli kuhusu Hila za Da Vinci?
Je, Yesu alisema kitu gani kinatokea baada ya sisi kufa?
Ikiwa ni kweli Yesu alifufuka toka katika Wafu, basi lazima ajue kitu gani kipo upande mwingine. Ni kitu gani alisema kuhusu maana ya maisha na siku zetu zijazo? Kuna njia nyingi kwenda kwa Mungu au Yesu alidai kuwa njia pekee? Soma majibu ya kushangaza “Kwanini Yesu?”
Bonyeza hapa kusoma “Kwanini Yesu?” na gundua kile Yesu alisema kihusucho maisha baada ya kifo.
Je, Yesu anaweza leta maana katika maisha?
“Kwanini Yesu? inaangalia suala la kwamba Yesu ni muhimu leo. Je, Yesu anaweza kujibu swali kubwa la maisha: “Mimi ni nani?” “Kwani niko hapa?” na, Wapi ninaenda?” Makanisa yaliyokufa na misalaba imewaongoza wengine kuamini kwamba hawezi, na kwamba Yesu ametuacha sisi kuendana na dunia iliyo nje ya uwezo wetu kuidhibiti. Lakini Yesu amefanya madai kuhusu maisha na madhumuni yetu hapa dunani ambayo yanahitaji kuchunguzwa kabla hatujamkataa kama asiyejali na asiye na nguvu. Makala hii inachunguza siri ya kwanini Yesu alikuja duniani.
Bonyeza hapa kwa ajili ya kudai zaidi fantastic milele alifanya – ya ufufuo wa Yesu Kristo!